tagumtwa

Blog hii inamilikiwa na Umoja wa Ukoo wa Kivenule

+ 0 - MAAZIMIO YA KIKAO KATI YA WAZIRI MKUU NA MADAKTARI LEO CPL"

In Tagumtwa Foundation on February 2, 2012 at 09:14

"MAAZIMIO YA KIKAO KATI YA WAZIRI MKUU NA MADAKTARI LEO CPL"

*TAARIFA KWA UMMA NA MADAKTARI WOTE NCHINI JUU YA MAAMUZI YALIYOFIKIWA
LEO FEBRUARY 9, 2012 KUFUATIA MKUTANO KATI YETU NA WAZIRI MKUU MHE.
MIZENGO PINDA KATIKA UKUMBI WA CPL, HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI*

Kamati ya muda ya kushughulikia madai ya madaktari nchini inapenda kuwajulisha madaktari wote pamoja na kada nyingine zote za afya nchini juu ya kile ambacho kimejiri katika siku ya leo ya tarehe 09.02.2012 ikiwa ni matokeo ya kikao wanataaluma wa kada za afya na Waziri Mkuu Mhe.
Mizengo Pinda na baadaye kufuatiwa na kikao kati ya madaktari na kada nyingine
za afya.

Ifahamike kuwa kama Kamati tulipata mwaliko wa kushiriki katika Mkutano huo ambapo ilitarajiwa kuwa Mhe, Waziri mkuu atafika kwa nia ya kutoa mrejesho wa madai ya madaktari yaliyowasilishwa mezani kwake mnamo tarehe 23.01.2012. Madai yetu yalikuwa manane na Mh Wazizri mkuu aliweza
kutoa maelezo ya dai moja baada ya lingine.

Miongoni mwa madai ambayo mpaka sasa yamepatiwa majibu ya kuridhisha ni pamoja na;

1. Kuwawajibisha watendaji wakuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, wakiwemo Katibu Mkuu Mama Blandina Nyoni, na Mganga Mkuu wa Serikali Dr. Deo Mtasiwa. Aidha Mh waziri mkuu alisema kuwa ameshalifikisha kwa Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania suala zima la kuwawajibisha watendaji wa wakuu wa kisiasa wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambao ni
Waziri Mh. Hadji Mponda na  Naibu Waziri  Mhe. Lucy Nkya.

2. Kama sehemu ya maridhiano, Mh Waziri Mkuu pia aliahidi mbele ya mkutano kuwa hakutawepo na unyanyasaji au vitisho vya aina yoyote ile kwa wale wote walioshiriki katika kushinikiza Serikali kutatua kero hizo. Aidha kama sehemu ya maridhiano, Mh waziri Mkuu pia alifuta zuio la madaktari kutokufanya mikutano. Lakini pia, Mh waziri Mkuu alisema kuwa Serikali haina kusudio la kumfukuza kazi mtumishi yeyote wa afya yule kazi aliyeshiriki katika mchakato huu wa kuishikiniza Serikali kutafuta ufumbuzi madai ya madaktari nchini.

3. Aidha, Mh waziri Mkuu amesema “Interns” wote waliokuwa wamehamishwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wamesharudishwa bila masharti katika hospitali hiyo ili kuendelea na program kama kawaida. Hili pia linaambatana na kulipwa na kupewa stahiki zao zote.

4. Pia suala la madaktari na familia zao kuwa na Kadi ya Bima ya Afya ya kijani (Green Card) limekubaliwa na kwa sasa tusubiri utekelezaji.

5. Pia ilikubaliwa kuwa madaktari watapata fursa ya kukopeshwa magari kama watumishi wengine wa umma.

Mbali na madai hayo, pia Mh. Waziri Mkuu alitoa ufafanuzi juu ya madai yanayuhusu maslahi ya watumishi wa afya ikiwa ni pamoja na Mishahara na Posho na stahiki mbalimbali. Lakini hata, Mh waziri Mkuu hakutoa majibu ya moja kwa moja ya kiwango gani kitakachoweza kulipwa na Serikali kama mishahara, posho na stahiki mbalimbali kwa minajili kwamba bado zinafanyiwa kazi na kamati ya wataalamu aliyoiunda ili waweze kumshauri. Aidha, Mh waziri Mkuu alisema kuwa kwa wakati huu inaweza kupandisha “on call allowances” za kada mbalimbali za afya kutoka shilingi 3,000 – 10,000/
= na kufikia kati ya shilingi 5,000 hadi 25,000. Madaktari bado wanaona ongezeko hili halilingani na ukubwa wa kazi ifanywayo pindi mtumishi wa afya anapokuwa “on call” na hivyo basi kuendelea kupendekeza kuwa “on call” allowance iwe ni 10% ya mshahara  wa mtumishi husika.

Pia Mhe, Waziri Mkuu hakuweza kueleza kinagaubaga mkakati kazi wa uboreshaji wa huduma za afya wapatayo wananchi wa Tanzania.

Baada ya tamko hilo la Serikali kumalizika, Mh Waziri Mkuu na ujumbe wake waliondoka, na Mkutano huo ukaendelea kwa Kamati kufanya Mkutano na madaktari wote, lengo ikiwa kujadili tamko hilo na kutoa maazimio. Baada ya majadiliano ya muda mrefu, madaktari walikubaliana kwamba; kwa kuwa Serikali imeanza kuonyesha nia ya kutatua tatizo hili kwa kutekeleza baadhi ya maazimio yetu, wajumbe kwa niaba ya madaktari wote nchi nzima tulikubaliana na kuazimia yafuatayo;

1. Kurudi kazini mara moja kuanzia kesho tarehe 10.02.2012 bila masharti yeyote.

2. Kamati ya jumuiya ya madaktari kama sehemu ya MAT kuendelea kukaa mezani ya majadiliano na Serikali ili kuanza kupitia madai hasa yale yanayohusu maslahi.

3. Kukutana tena tarehe 03.03.2012 ili kupata mrejesho wa kiwango cha utekelezaji wa madai hayo kwa mujibu wa vikao vya majadiliano na makubaliano na hatimae kuchukua hatua zaidi.

4. Kujadili utekelezaji juu ya Kuwawajibisha Waziri na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi na Jamii.

5. Mwisho kabisa Madaktari wote kwa ujumla wake walilaani na kukemea kitendo cha Jeshi la Polisi kuwakamata na kuwahoji wanaharakati wa haki za kibinaadamu na mashirika ya kijamii wakiwemo Dr. Hellen Kijo-Bisimba na Mama Ananilea Nkya na wanaharakati wengine wote waliokumbwa na
kamata kamata hiyo na hivyo basi tunalitaka jeshi hilo kuwaachilia huru mara moja bila masharti yeyoye.

Pamoja Tunaweza

Imetolewa na Kamati ya muda ya kushughulikia madai ya madaktari Tanzania

 

Dr, Ulimboka Stephen

Mwenyekiti.

 


Tags : maazimio - kikao - kati - waziri - mkuu - madaktari - leo - cpl

+ 0 - Activists demand government action to resolve health crisis or resign

In Tagumtwa Foundation on February 2, 2012 at 09:32

Activists demand government action to resolve health crisis or resign

Thirteen leaders of national and grassroots activist organizations in Tanzania have been detained today by the government in the Oyster Bay Police Station, Dar es Salaam, in a government clamp down on protests
by women/feminist and human rights activists against the failure of the government to resolve the health crisis arising from a two week doctors strike in Tanzania. The leaders come from LHRC, TGNP, TAMWA, NEDPHA and several other  grassroots organizations. They and others were on their way to Muhimbili Hospital to await the outcome of talks
which the Prime Minister was having with striking doctors. On Wednesday 8th February more than 200 activists successfully ‘occupied’ Salendar Bridge and the roads leading into it for two hours, and got major media attention and support from motorists and passersby for their action, based on the posters demanding that the Minister of Health and other top officials must resign; and protesting the failure
of the President’s Office and the Parliament to give the situation priority. Countless numbers of people have died as a result of the strike. However, as the participating organizations such as TGNP have
noted, people were dying long before this strike because of the lack of adequate human, financial and material resources provided to health
care at all levels.

Many of the organizations leading the protest are members of the Feminist Activist Coalition, Fem Act, including TGNP, TAMWA, LHRC, HakiElimu, SIKIKA, and NEDPHA; others belong to Policy Forum, including  Policy Forum itself; and many others are grassroots
organisations participating in the Gender and Development Seminar Series [GDSS].

Marjorie Mbilinyi, TGNP


Tags : activists - demand - government - action - resolve - health - crisis - resign

+ 0 - HALI INAVYOTISHA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MUHIMBILI

In Tagumtwa Foundation on February 2, 2012 at 16:31

Breaking News!

HALI INAVYOTISHA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MUHIMBILI

Taarifa zilizopatikana kupitia ziara ya Wanaharakati waliotembelea Hospitali ya Rufaa Muhimbili zinasikitisha kwa kila Mtanzania ambaye ana uchungu wa nchi hii na Watanzania. Picha zilizopigwa zinaonesha hali halisi ya mazingira ya hospitali hiyo ambayo ni kubwa kuliko zote hapa Tanzania inavyotisha, huku wagonjwa wakiendelea kuteseka kwa taabu na kukosa huduma za matibabu na utabibu mwingine ambao walipaswa kuupata.

Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili ni hospitali kubwa kuliko zote hapa Tanzania Bara na Visiwani. Ni sehemu ambapo wagonjwa toka kona zote za Tanzania Bara na Visiwani hufika hapa kupata matibabu pale inapokuwa imeshindikana kutoka hospitali nyingine.

Hospitali hiyo inaaminika kwa kushesheheni Waganga na Wataalam wa Tiba wenye weledi na umahiri wa kina aina. Ina Madaktari Bingwa ambapo ni tegemeo la Watanzania walio wengi ambao hawana uwezo wa kwenda kutibiwa nje ya nchi kama wanafanya viongozi wa nchi yetu.

Athari za serikali kushindwa kusikiliza kilio cha Waganga hao ambao ndio tegemeo la uhai wa taifa hili, ndizo zinazojitokeza katika hospitali ya Muhimbili. Natumaini Watanzania wengi wataumia kwa kuona hali halisi ilivyo kwa wagonjwa wetu ambao muda huu wanaendelea kuteseka na pengine kujuta kuwa kuzaliwa katika nchi yetu ambayo ilikuwa na historia ya kujali utu na kuheshimu haki za Binadamu.

Bonyeza Linki hii:

 ili ujionee hali ilivyo katika hospitali ya Muhimbili. Pia utawaona wanaharakati ambao wanajitahidi kuutaarifu umma hali ilivyo kwa sasa.

Imeandaliwa na:

 

Adam Kivenule

KAUKI


Tags : hali - inavyotisha - katika - hospitali - rufaa - muhimbili

+ 0 - SITUATION IN MUHIMBILI REFERRAL HOSPITAL SCARE

In Tagumtwa Foundation on February 2, 2012 at 16:29

Breaking News!

SITUATION IN MUHIMBILI REFERRAL HOSPITAL SCARE

Information obtained through the visit of activists who visited Muhimbili Referral Hospital is irritating for every Tanzanian who has the pain of this country and her people.  Pictures taken show the reality of the situation of the hospital, which is the largest in Tanzania, while patients continue to suffer misery, dying and lack of medical care and other medical personnel who were supposed to attend them.

Muhimbili Referral Hospital is the largest hospital in Tanzania Mainland and Zanzibar.  It is a place where patients from all corners of Tanzania Mainland and Zanzibar are coming here to get services when they did not secure the required treatments from other hospitals.

The hospital posses a qualified Medical and Therapy Professionals with professionalism and competence of the extensive diversity.  Doctors Champion which has indisputably the majority of Tanzanians who can not afford to go abroad to be treated like they do the leaders of our country.

The impacts of government failure to listen to the cries of Doctors is a source of strike which indisputably threaten life of people of this nation, as witnessed at the Muhimbili hospital.  I hope majority will suffer by seeing reality for our patients that continue to die perhaps regret being born in our country which had a history of caring for the dignity and respect human rights.

 Click on this link:

http://www.facebook.com/media/set/?set=a.318692444848583.90342.129370793780750&type=1&l=924a1f62b8

Prepared by:

 

Adam Kivenule

KAUKI

 

 


Tags : hali - inavyotisha - katika - hospitali - rufaa - muhimbili - situation - referral - hospital - scare

+ 0 - MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2011 YAMETOKA - KIDAMALI

In Tagumtwa Foundation on February 2, 2012 at 14:02

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2011 YAMETOKA - KIDAMALI

Matokeo ya Kidato cha Nne kwa Mwaka 2011 yametoka. Kwa wenzetu kutoka Kidamali, wanaweza kupata matokeo ya Shule ya Sekondari ya Kidamali kupitia linki ifuatayo: http://196.44.162.14/necta2011/CSEE%202011/s3635.htm

 

Imewekwa na:

 

Adam Kivenule

KATIBU - KAUKI

 

 


Tags : matokeo - kidato - cha - nne - 2011 - yametoka - kidamali

+ 0 - MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2011 YAMETOKA

In Tagumtwa Foundation on February 2, 2012 at 13:54

 MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2011 YAMETOKA

Matokeo ya Kidato cha Nne mwaka 2011 kwa Watahiniwa waliofanya Mtihani wa Kuhitimu Kidato cha Nne nchini Tanzania yametangazwa kwenye tovuti ya Baraza la Mitihani la Taifa - NECTA. Kwa taarifa zaidi tembelea linki hii http://www.necta.go.tz/

 

 

 

Imetolewa na:

 

Adam Kivenule

Katibu - KAUKI

 


Tags : matokeo - kidato - cha - nne - 2011 - yametoka

+ 0 - ADVERTISEMENT

In Tagumtwa Foundation on February 2, 2012 at 09:07

Announcement

Dear All,

Tanzania Transparency Forum (TRAFO) in collaborating with Transparency International Kenya (TI-Kenya) is planning to build (create) a National Database of Research Assistants in Tanzania. The database will support TRAFO and TI-Kenya to recruit Research Assistants on need basis for different short term projects.  We invite applications for interested persons.  The minimum requirements for those interested their names to be included in the database are as follows:-

  • Second or third year university student in a recognized local university studying Arts / Social Sciences;
  • Able and willing to be deployed on various research projects by TRAFO and TI-Kenya sometimes on short notice;
  • Generally conversant with the geography of the areas around the university/ college and / or region of residence;
  • Good communication skills; and
  • Willingness and ability to travel widely across the area allocated.

Inclusion into the database does not create liability on the part of TRAFO or TI-Kenya to provide opportunity during any research assignment. Any engagement will be based on tasks available, number of research assistants required and general suitability of the research assistant.

Interested students are required  to forward their applications indicating their geographical regions and C.Vs by January 24th, 2012 to the following address:

Assistant Programme - TRAFO

Off University Road, Survey Area, Kawe/Mlalakuwa Plot # 301-304, House # 250

P.O. Box 32505,

Dar es Salaam -TANZANIA

Tel:  +255 22 2701890

        +255 22 2701895-6

Cell: +255 784 410 939

Fax: +255 22 2701890

E-mail: Tanzaniatransparencyforum-TRAFO@fordia.org/juliette.kingalu@fordia.org/ info@fordia.org 

Website: www.fordia.org 

 


Tags : advertisement

+ 0 - KADI YA OMBI LA MCHANGO WA MKUTANO WA 8 WA KAUKI

In Tagumtwa Foundation on February 2, 2012 at 12:17

KADI YA OMBI LA MCHANGO WA MKUTANO WA 8 WA KAUKI


Tags : kadi - ombi - mchango - mkutano - kauki

+ 0 - RATIBA YA MKUTANO MKUU WA NANE WA KAUKI

In Tagumtwa Foundation on February 2, 2012 at 11:37

RATIBA YA MKUTANO MKUU WA NANE

WA UMOJA WA UKOO WA KIVENULE-KAUKI

Siku ya Kwanza ya Mkutano Mkuu – Dar es Salaam: Tarehe 30 Juni 2012

Muda

Shughuli/Jukumu

Wahusika

12.00 – 12.45

Wageni Wote Kuamka na Kufanya Maandalizi ya Kuingia kwenye Mkutano

Wote

12.45 – 01.15

Kupata Kifungua Kinywa

Washiriki wote

01:15 – 02:00

Kuwasili Mkutanoni na Kujisajili na kupata vitambulisho

Washiriki wote

02.00 – 02.20

Kusoma Hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Nane wa KAUKI

Mwenyekiti wa KAUKI

02.20-02.45

Ufunguzi Rasmi wa Mkutano na Mgeni Rasmi

Mgeni Rasmi

02.45-03.15

Utambulisho baina wa Ndugu na Wageni Waalikuwa

Wote

03.15 – 04:00

Mada: CHIMBUKO, HISTORIA NA MUUNDO WA UKOO WA KIVENULE

(a). Washiriki wasambaziwe nakala ya muundo wa Ukoo na kisha kuujadili na kutoa mawazo yao katika makundi

Mwakilishi toka  Kidamali

Mwakilishi toka Ilole 

mwakilishi toka Nduli

Washiriki wote

Mtaalam wa Historia

04:00– 04:30

Pumziko la Chai / Kahawa/Maji

Washiriki Wote

04.30-04.45

Mada Inaendelea.

(b). Washiriki waijadili mada na kutoa mapendekezo

(c). Washiriki waijadili mada na kupendekeza nini kifanyike kutunza kumbukumbu hizo

(d). Washiriki wazijadili njia mbadala za kutunza taarifa zinazohusiana na ukoo

Wawezeshaji na Washiriki wote

04.45-05.05

Kuwasilisha majadiliano katika Makundi

Washiriki wote na Wawezeshaji

05.05-05.30

Majumuisho ya yote yaliyojitokeza katika Mada

Wawezeshaji

05:30 – 06:30

TAARIFA YA UTENDAJI WA KAUKI:

1. Mipango na Shughuli zilizokusudiwa kufanywa na KAUKI 2011/2012;

2. Taarifa ya Utendaji kwa Ujumla;

3. Taarifa ya Mahesabu na Fedha; na

  1. Mafanikio na Matatizo ya KAUKI

4. Matarajio ya KAUKI 2010/2011

Makamu Katibu Mkuu

Mhasibu

06.30 – 07.00

TAARIFA YA SHUGHULI ZA MAENDELEO KATIKA KANDA

1. Uhamasishaji

2. Mwitikio wa Jamii inayounda Ukoo

3. Ushirikiano miongoni mwa wanajamii

4. Mafanikio na Matatizo

Viongozi wa Kanda zote

07.00-08.00

CHAKULA CHA MCHANA

Washiriki wote

8:00 – 8:45

KUSOMA RIPOTI YA MKUTANO MKUU WA SABA WA KAUKI

Kujadili Mapungufu, Kutoa Ushauri, Nyongeza

Kupitisha Ripoti

Katibu Msaidizi

Washiriki wote

08:45 – 09:15

Salaam mbalimbali kutoka kwa Washiriki wa Mkutano Mkuu (Wastani watu 6 na dakika @ 5)

Washiriki wa Mkutano

09:15– 09:45

Pumziko la Chai/Kahawa/Maji

Washiriki wote

09.45 -11:00

UZOEFU WA WANAUKOO KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO

1.Kidamali/Magubike: Kilimo cha Nyanya /Tumbaku na shughuli nyingine za kiuchumi dakika 25

2. Irole/Nduli/Itagutwa/Mgongo: Uzoefu wa Shughuli za Kiuchumi dakika 25

3. Dar/ Morogoro/ Kilombero / Moshi dakika 15

4. Kalenga, Ifunda, Ilala Simba, Wasa, Idodi na Nyamihuu

Washiriki wote; viongozi wa Kanda au wajumbe watakaochaguliwa kutoa uzoefu wa shughuli hizo za kiuchumi

11.00

KUAHIRISHA MKUTANO

Mwenyekiti wa KAUKI

2:30 – 6:30 Usiku

Burudani (Muziki wa Kisasa na Ngoma za Asili), vinywaji, kufahamiana zaidi na kubadilisha mawazo

Wanaukoo wote

 

Siku ya Pili ya Mkutano Mkuu – Dar es Salaam: Tarehe 01 Julai 2012

Muda

Shughuli/Jukumu

Wahusika

12.00 – 12.45

Wageni Wote Kuamka na Kufanya Maandalizi ya Kuingia kwenye Mkutano

Wote

12.45 – 01.15

Kupata Kifungua Kinywa

Washiriki wote

01:15 – 02:00

Kuwasili Mkutanoni na Kujisajili

Washiriki wote

 

02.00-02.45

MADA: CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI KAUKI KUJILETEA MAENDELEO

1. Nini kifanyike kwa wana-KAUKI kujiletea Maendeleo?

2. Mnadhani ni vitu gani vipewe Kipaumbele kwa wanaukoo kunufaika na KAUKI!

3. Baadhi ya Malengo ya KAUKI ambayo mnayafahamu mnadhani yatasaidia kuleta mabadiliko? Na ni kwa namna gani? Jadili

4. KAUKI ni sehemu tu ya vikundi vingi vinavyofanya jitihada za kujiinua kiuchumi na kimaendeleo, mnadhani ni changamoto gani tunaipata ukilinganisha na mafanikio au matatizo ambayo yamevipata vikundi vingine? Yajadili na kuyatoa mapendekezo hayo

Wawezeshaji na washiriki wote

02.45-03.15

Majadiliano katika Makundi : Kila mshiriki ajidiliane na wana kundi kikamilifu na kutoa hoja za msingi za kujenga. Kila hoja ya msingi iwasilishwe ila kila mwanaukoo asikie.

Washiriki wote wagawanyike katika makundi

03.15-03.45

Makundi kuwasilisha hoja kutoka katika makundi yao

 

Washiriki wote

03.45-04.30

Majumuisho ya yote yaliyojitekeza katika Mada

Wawezeshaji

04:30 – 05:00

Pumziko la Chai / Kahawa/Maji

Washiriki Wote

05.00-06.00

HISTORIA YA WAHEHE

  1. Kuibuka kwa tawala mbalimbali ndani ya Uhehe (Wanitole, Wahabeshi, Wangazija)
  2. Chimbuko la Koo mbalimbali mkoani Iringa
  3. Mahusiano yaliyopo baina ya koo zilizoibuka wakati wa vita za kikabila na wageni
  4. Mgawanyiko wa Koo katika Mkoa wa Iringa

 

Washiriki wote na Viongozi wa KAUKI

06.00-07.00

MAHITAJI YA KAUKI NA JINSI YA KUFANIKISHA KUPATIKANA KWA MAHITAJI HAYO: Huu ni mjadala wa jumla na kila mjumbe wa mkutano anashiriki moja kwa moja kutoa mawazo yake. Katibu na watendaji wengine wa KAUKI wana jukumu ya kuyanakili maswali na majibu yote kwa ajili ya kufanyiwa kazi

Washiriki na Viongozi wa KAUKI

 

 

 

07.00-08.00

CHAKULA CHA MCHANA

Washiriki wote

08:00–08.20

MAJADILIANO YA HOJA MBALIMBALI AMBAZO ZIMEWASIISHWA NA WASHIRIKI WA MKUTANONI

 

08:20 - 8:40

  1. MAJUMUISHO NA TATHMINI YA MKUTANO
  2. MIPANGO NA MIKAKATI YA MBELENI
  3. KUTANGAZWA KWA TAREHE YA MKUTANO MKUU WA TISA

VIONGOZI WA KAUKI

8:40 - 9:00

UCHAGUZI WA VIONGOZI WA KAUKI

Washiriki Wote

09.00-09:15

SHUKRANI NA KUFUNGA MKUTANO

VIONGOZI WA KAUKI NA MGENI RASMI

09:15–09:30

Pumziko la Chai/Kahawa/Maji

Washiriki wote

09:30

ZIARA YA KUTEMBELEA JIJI LA DA RES SALAAM KWA WAGENI WOTE. Maeneo ambayo yatatembelwa ni pamoja na:

Eneo Kariakoo, Katikati ya Mji, Bahari (Koko Beach), Mlimani City na Chuo Kikuu

Washiriki Wote

 

 


Tags : kauki - ratiba - mkutano - mkuu - nane

+ 0 - OMBI LA MCHANGO WA KUFANIKISHA MKUTANO MKUU WA 8 WA KAUKI

In Tagumtwa Foundation on February 2, 2012 at 09:34

OMBI LA MCHANGO WA KUFANIKISHA MKUTANO MKUU WA 8 WA KAUKIOMBI LA MCHANGO WA KUFANIKISHA MKUTANO MKUU WA 8 WA KAUKI


Tags : tangazo - ombi - mchango - kufanikisha - mkutano - mkuu - kauki

Blog Labels

umoja - nane - tanzia - historia - magubike - nne - pili - scare - leo - crisis - clan - kikao - resolve - yametoka - government - kwa - 0 - mashauriano - michango - ruaha - chimbuko - kanda - mikutano - ombi - kidamali - activists - salaam - mkutano - 1 - soka - madaktari - mwaliko - maazimio - tanzania - viongozi - mchango - taarifa - matukio - sita - muhimbili - hospitali - wakati - demand - kwanza - resign - maandalizi - dar - ukoo - matokeo - moja - picha - kidato - kauki - julai - kufanikisha - tangazo - jijini - ratiba - country - barua - national - michezo - for - hotuba - 2 - 3 - mkuu - waziri - action - uingereza - referral - kitabu - nini - katika - video - losina - desemba - saba - ufunguzi - wana - kivenule - 4 - cpl - cha - muundo - marehemu - park - hospital - youtube - advertisement - kati - kadi - rufaa - nembo - maendeleo - ripoti - iringa - mufindi - kufanyika - namibia - health - igowole - situation - inavyotisha - juni - bango - tree - hali - wanaukoo - 5 - kilimanjaro

Platted Hairstyles For Men
The basic purpose of any hairstyle should be to add liveliness and create an effect.
www.lastsee.com